Responsive image
Responsive image
Posted : December 22, 2017 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Tanzania imeporomoka kwa nafasi tano kwenye viwango vya soka vya shirikisho la soka Duniani FIFA kwa mwezi Novemba.

Kwa mujibu wa taarifa ya viwango hivyo iliyotolewa leo na FIFA,Tanzania imeporomoka hadi katika nafasi ya 147 kutoka nafasi ya 142 iliyokuwepo mwezi Oktoba.

Kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki, Uganda imeendelea kuongoza ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani ikifuatiwa na Kenya iliyopanda kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 111 hadi 106 na Rwanda iliyopanda kwa nafasi saba kutoka nafasi ya 120 hadi katika nafasi ya 113.

Senegal inaendelea kuongoza barani Afrika ikiwa inakamata nafasi ya 23 Duniani ikifuatiwa na Tunisia, Misri, Jamhuri Ya Kidemokrasi Ya Kongo, Morocco, Burkina Faso, Cameroon, Ghana , Nigeria Na Algeria.

 

ASHER THOMAS

22 DESEMBA 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment