Responsive image
Responsive image
Posted : December 20, 2017 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Mashuhuda wa ajali wakifanya zoezi la uokoaji
Responsive image

Watu saba wamekufa na wengine 18 kujeruhiwa katika  ajali iliyohusisha basi lenye namba za  usajili T384 BMG mali ya kampuni ya Saratoga na toyota Hiace yenye namba za uasajili  T237BCE mali ya Hassan Rajab.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi  mkoa wa Kigoma Filbert Njoike basi la Saratoga lilikuwa likisafiri kutoka Sigunga kwenda Kigoma mjini wakati Hiace ilikuwa ikitokea Kigoma mjini Kwenda Ilagala.

Kamanda huyo amesema ajali hiyo  imetokea katika kijiji cha Kabeba kata ya Mwakizega wilayani Uvinza  na kwamba chanzo cha ajali ni mwendo kasi uliosababisha madereva hao kushindwa kumudu magari yao .

Katika kitua cha afya cha Ilagala ambapo wahanga wa ajali hiyo wamefikishwa umati wa watu uliogubikwa na nyuso za huzuni ulifurika,  ambapo mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Vitus Bukombe amethibitisha kupokea majeruhi.

EGIDIUS AUDAX

DISEMBA 201, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment