Responsive image
Responsive image
Posted : December 17, 2017 (4 months ago) By TBC
Responsive image
George Mkuchika
Responsive image

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Utumishi wa Umma Kapteni mstaafiu George Mkuchika ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kuwa shilingi milioni 123 zilizolipwa kwa watu wasiostahili kupitia mpango wa maendeleo ya jamii TASAF awamu ya tatu.zinarejeshwa  haraka.

Kapteni Mkuchika amesema kuwa pamoja na uamuzi uliochukuliwa na uongozi wa mkoa huo wa kuwaachisha kazi watendaji wa mitaa na kata waliohusika na tuhuma hizo za fedha walipaswa kurejesha fedha hizo

Agizo hilo amelitoa  wakati  akizungumza kwa nyakati tofauti na viongozi wa mitaa, kata na viongozi wa Wilaya na Mkoa  huku akiwataka watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi ya umma .

DOTTO              ELIAS

DISEMBA 17, 2017  

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment