Responsive image
Responsive image
Posted : December 16, 2017 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Wananchi wa vijiji vya Membe na Mlimwa, Chamwino Dodoma wakimsikiliza waziri Lukuvi (hayupo pichani)
Responsive image

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amefuta uamuzi wa viongozi wa vijiji vya Membe na Mlimwa vilivyopo Kata ya Membe Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wa kumpatia ardhi yenye ukubwa wa ekari 1,756 mwekezaji David Mazoya Poli tangu miaka 10 iliyopita hali iliyosababisha mgogoro wa ardhi na kuhatarisha amani katika Kata hiyo.

Akizungumza na wakazi wa Kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara waziri Lukuvi amesema amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na serikali za vijiji hivyo kwani yalikiuka Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 inayotoa mamlaka kwa Vijiji kumilikisha ardhi isiyozidi ekari 50. .

Mwekezaji huyo alimilikishwa ardhi hiyo ikiwemo ekari 100 alizopewa na Kijiji cha Membe kwa makubaliano kuwa angewajengea Ofisi ya Serikali ya Kijiji ahadi ambayo hata hivyo hajaitekeleza.

Wakazi wa Kata hiyo wamemshukuru waziri Lukuvi kwa uamuzi huo wa Serikali kwa madai kwamba wameteseka kwa kipindi kirefu ikiwa ni pamoja na kukosa maeneo ya kulima na malisho kwa ajili ya mifugo yao.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment