Responsive image
Responsive image
Posted : December 15, 2017 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihojiwa na mwandishi wa TBC Mbozi Katala
Responsive image

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma kumuunga mkono katika kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa kupanda miti.

Makamu wa Rais ametoa wito huo leo katika  tafrija ya kumkaribisha  rasmi makao makuu ya nchi mjini Dodoma.

 Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani  kutumia nafasi ya serikali kuhamia Dodoma kubaini fursa za kibiashara ili kujipatia kipato huku akisema kuwa serikali inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo ujenzi wa kituo cha kisasa cha mabasi ili kurahisisha usafiri.

 Katika kutimiza agizo la  Rais Dkt John Magufuli la serikali kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma  leo makamu wa rais Samia Suluhu amehamia Dodoma, baada ya waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhamia  Septemba 30 mwaka jana.

Inatarajiwa kuwa muda wowote kuanzia sasa hadi mwishoni mwa mwaka 2019 rais pia atahamia Dodoma.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment