Responsive image
Responsive image
Posted : December 07, 2017 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Jakaya Kikwete
Responsive image

Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar es salaam Dokta Jakaya Kikwete amemsimika rasmi Profesa William Anangisye kuwa makamu mkuu wa chuo hicho kuchukua nafasi ya Profesa Rwekaza Mukandala aliyemaliza muda wake.

Akizungumza katika hafla ya kumsimika Makamu mkuu huyo wa chuo Dkt Kikwete amemtaka makamu huyo kufanya kazi kwa ushirikiano na wafanyakazi wengine ili kuongeza  ufanisi. 

Kwa upande wa Makamu mkuu wa chuo aliyemaliza muda wake Profesa Mukandara amesema chuo hicho kimefanikiwa kuwa chuo kilichotoa viongozi wa hapa nchini na nchi mbalimbali barani Afrika.

Naye makamu mkuu wa chuo hicho Profesa  Anangisye ameahidi kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho kukifanya kuwa sehemu ya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu ili kutatua changamoto zinazoikabili serikali na jamii kwa ujumla. 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment