Responsive image
Responsive image
Posted : December 07, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Mwandishi wa habari Azory Gwanda aliyepotea siku 17 zilizopita
Responsive image

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji, Onesmo Lyanga amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio la kupotea kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda.

Akizungumza na TBC Kamanda Lyanga amesema bado hawajabaini chochote kwa vile mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo ni ya utata kutokana na  kwamba aliweza kumuaga mkewe na hapakuashiria kama kulikuwa na hali isiyo ya usalama. 

“Bado tunaendela na uchunguzi na hadi wakati huu hatujabaini chochote, mwandishi huyo alikuwa akifika  ofisini kwetu akitaka taarifa na tulikuwa tunampa ushirikiano”amesema Lyanga

Leo ni siku ya 17 tangu mwandishi huyo wa gazeti la Mwananchi apotee ambapo kwa mujibu wa Kamanda Lyanga jalada la kupotea kwake limefunguliwa polisi .

Kwa mujibu wa mke wa  mwandishi huyo Anna Pinoni watu wapatao wanne wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walimchukua bwana Gwanda kutoka katikati ya mji wa Kibiti, mahali ambapo hupendelea kukaa.

Ameripotiwa akisema pia kwamba aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ikiwa ni ishara kwamba nyumba yao ilipekuliwa.

 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment