Responsive image
Responsive image
Posted : December 06, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Manyara mstaafu Dkt Joel Bendera
Responsive image

Mkuu wa mkoa mstaafu wa Manyara, Dkt Joel Bendera amefariki dunia leo jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam alikopelekwa kwa matibabu akitokea Bagamoyo mkoani Pwani.

Kufuatia kifo hicho Rais John Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia yake na wote walioguswa na msiba huo na kusema anaungana nao katika kipindi hiki cha msiba.

Katika salamu zake za rambirambi Rais Magufuli amesema Dkt. Bendera atakumbukwa kwa mchango wake kwa taifa akiwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge, Naibu Waziri na mchango wake katika sekta ya michezo.

Pamoja na salamu hizo ametoa pole kwa wananchi wa mkoa wa Manyara akipokuwa Mkuu wa mkoa hadi Oktoba 26 mwaka huu, wananchi wa Tanga ambapo alikuwa mbunge, wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi na wanamichezo wote.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment