Responsive image
Responsive image
Posted : December 06, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi sita za taasisi za serikali baada ya wenyeviti waliokuwepo kumaliza muda wao.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imewataja walioteuliwa kuwa ni Monica Mbega anayekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Profesa Egid Mubofu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania –TFC, Profesa Abiud Kaswamila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Profesa Esther Jason kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, DktKenneth Mdadila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya kifedha ya Self Microfinance Fund Limited na Dkt. Titus Kamani kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment