Responsive image
Responsive image
Posted : December 06, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (aliyevaa suti ya rangi ya bluu) akikagua jengo litakalotumiwa na Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan
Responsive image

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua maendeleo ya matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan  atakapohamia Dodoma.

 Waziri Mkuu amefanya ukaguzi huo leo mchana  katika eneo la Kilimani, mjini Dodoma .

Waziri Mkuu pia amekagua matengenezo ya Ofisi inayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais itakayokuwa  eneo la Ndejengwa.

 Naye Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dodoma ambaye anasimamia ujenzi huo Steven Simba, amesema  kuwa  kazi hiyo itakamilika kabla ya Desemba 30, mwaka huu.

Kazi ya matengenezo kwenye makazi ya makamu wa rais itagharimu Sh. bilioni 1.5 wakati kazi ya kutenganisha ofisi za watumishi na wasaidizi wa Makamu wa Rais itagharimu sh. milioni 680.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment