Responsive image
Responsive image
Posted : December 06, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Benki ya TIB imetoa msaada wa vifaa tiba vevye thamani ya shilingi milioni saba katika zahanati ya Msongola wilayani Ilala Jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIB ,Edward Lyimo amesema benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kutoa sehemu ya mapato yake ili kuisaidia jamii inayowazunguka.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameipongeza benki hiyo na kuitaka jamii kuwa na moyo wa kuchangia huduma za afya na kwamba mkakati wa serikali ni kuhakikisha hakuna vifo vinavyotokana na changamoto za uzazi ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara amesema upatikanaji wa vifaa vya kujifungulia utasaidia wananchi kuondokana na adha ya kufuata matibabu katika maeneo ya mbali.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment