Responsive image
Responsive image
Posted : December 05, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli akiwa na wawakilishi wa kampuni ya Total
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli amekutana na viongozi wa kampuni ya TOTAL ambayo ni mwekezaji mkubwa wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania na kuwahakikishia kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kwa kampuni hiyo na washirika wengine katika ujenzi wa mradi huo.

Baada ya mazungumzo hayo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wamesema viongozi wa Total wameamua kuimarisha soko la mafuta Tanzania na pia kushirikiana na Serikali katika utafiti wa mafuta katika maeneo ya Ziwa Tanganyika, Eyasi Wembere na Ziwa Rukwa.

 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment