Responsive image
Responsive image
Posted : December 05, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya raia wakishusha samaki
Responsive image

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera kwa kushirikiana na idara ya uvuvi Mkoani humo linawashikilia watu wawili akiwemo afisa ukaguzi wa mpaka wa Murusagamba Ayoub Ng’oma kwa tuhuma za kutaka kutorosha zaidi ya tani tatu  za samaki wabichi aina ya sangara na sato  kwenda nchini Burundi.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na jitihada zilizofanywa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngara ambayo ilifanikiwa kulikamata gari hilo likiwa limekwisharuhusiwa kutoka katika kituo cha ukaguzi cha mpaka huo.

Afisa uvuvi mkoa wa Kagera, Efraz Mkama anasema  wasafirishaji wamekiuka sheria ya uvuvi namba 22  ya mwaka 2003 inayomzuia mtu yeyote kusafirisha samaki ambao bado hawajachakatwa nje ya nchi.

Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele anawataka maafisa waliopewa dhamana ya kulinda maliasili za nchi kufanya kazi kwa kufuata sheria na maadili

CHARLES MWEBEYA

DISEMBA O5

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment