Responsive image
Responsive image
Posted : December 05, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani
Responsive image

Wilaya ya Misungwi imeelezwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa miradi ya REA ikilinganishwa na Wilaya nyingine nchini kutokana na kasi ya mkandarasi wa mradi huo ya kusambaza umeme.

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amepongeza jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa hatua yake ya kumsimamia mwekezaji na kumuagiza Meneja wa TANESCO Wilayani humo kufungua ofisi katika Kata ya Mwaniko na Mondo ili kuwahudumia wananchi kwa karibu.

Akikagua utekelezaji wa mradi wa REA katika Kata Ya Mwaniko na Mondo Waziri Kalemani ameelezea kufurahishwa kwake na kasi ya mkandarasi ya kusambaza umeme katika kata hizo.

Naye Meneja wa TANESCO Tawi la Mwanza   Mhandisi  Sarah Assey amesema licha ya ukamilishaji wa mradi huo kufikia vijiji ishirini na mbili lakini  Shirika la umeme pia litaweza kuongeza mapato kwa kuongeza  idadi ya wateja.

Tangu mwaka 2015 vijiji vilivyonufaika na mradi wa REA nchini vimeongezeka maradufu kutoka asilimia 21 hadi kufikia asilimia 49 mwaka huu, lengo likiwa ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 vijiji vyote 12,378 nchini vinapata umeme.

REGINALD NDESIKA 

DISEMBA 05, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment