Responsive image
Responsive image
Posted : December 04, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akohijiwa katika kipindi cha 'Tunatekeleza'
Responsive image

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema hakuna mgao wa umeme nchini na kwamba kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali kunasababishwa na ukarabati wa mitambo katika vituo vya kuzalishia umeme nchini lengo likiwa ni kufanya nchi iwe na umeme wa uhakika.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo leo katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na kituo cha televisheni cha  taifa TBC1.

“Mimi sipendi kuwepo kwa mgao wa umeme nchini, kinachofanyika ni matengenezo ya mitambo kwa kuwa mitambo tunayoitumia ni ya miaka mingi hivyo hadi kufikia Disemba 15 mwaka huu mambo yatakuwa mazuri tunawaomba wananchi watuvumilie” – Amesema Dkt. Kalemani.

Kwa muda sasa katika maeneo mengi nchini kumekuwepo na kero ya kukatika kwa umeme mara kwa mara jambo ambalo limekuwa likileta usumbufu kwa wananchi kutimiza majukumu yao.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment