Responsive image
Responsive image
Posted : December 04, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
Responsive image

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameunda timu ya watu watano kuchunguza sakata la kampuni ya NICO kupata hasara kwa kipindi cha miaka mitano tangu ilipoingia mkataba wa kuendesha kiwanda na machinjio ya kisasa ya Kizota mkoani Dodoma.

Akizungumza mkoani Dodoma alipotembelea machinjio hayo Waziri Mpina amesema endapo timu hiyo itabaini  masharti ya mkataba ya hayajatekelezwa serikali itavunja mkataba huo na kuyaweka machinjio chini ya kampuni ya ranchi ya Taifa – NARCO.

Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi Kampuni ya nyama TMC, Nathan Kalinga,amesema wanatarajia kuuza nyama nchi za kiaraabu baada ya kusimama kwa muda.

 

SHABAN   KWAKA                                                       

DISEMBA 04, 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment