Responsive image
Responsive image
Posted : November 30, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania bara The Kilimanjaro  Stars,  Ammy Ninje amesema  mipango yake ni kuchukua ubingwa wa michuano ya  kombe la CECAFA Senior Challenge inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 3 mwaka huu huko nchini Kenya.

Ninje amesema Kilimanjaro Stars inauwezo wa kutwaa taji hilo kwa sasa na endapo watatwaa taji hilo anaamini itaamsha morali katika harakati za kukuza  soka hapa nchini.

Pia kocha huyo amesema kila mchezaji kwenye kikosi hicho ana nafasi ya kucheza kwenye michuano hiyo na sio baadhi tu ya wachezaji wanaoweza kucheza.

``Nimeita wachezaji vijana sio kwamba hawana nafasi ya kucheza hapana watacheza tu kwasababu kuna michezo mingi na wao wanaweza kupambana `` amesema Ninje.

Pia kocha huyo amesema hajaona changamoto yeyote kwake katika kuinoa timu hiyo ingawa ni mara yake ya kwanza kufundisha timu ya Taifa na yeye kama kocha anatimiza kila anachotakiwa kukifanya kwa wachezaji wake.

Nahodha wa timu hiyo Himid Mau atajiunga na wenzie huko nchini Kenya kwa sababu hivi sasa yuko Afrika Kusini alikoenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Kilimanjaro Stars inaondoka leo kwenda nchini Kenya tayari kwa michuano hiyo ya 'Challenge' na imepangwa kwenye kundi A pamoja na timu za Kenya ambao ni wenyeji,Libya,Rwanda na Zanzibar.

EVANCE MHANDO

NOVEMBA 30, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment