Responsive image
Responsive image
Posted : November 28, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Uhuru Kenyatta akiapishwa
Responsive image

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameapishwa kuliongoza taifa hilo kwa miaka Mitano ijayo. Sherehe za kuapishwa Rais Kenyatta zimefanyika katika Uwanja wa Moi Kasarani Jijini Nairobi, ambapo William Rutto pia ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Kenya.

Wageni mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Rutto, akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amemwakilisha Rais John Magufuli .

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Haile Mariam Desalegn, Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Rais Ian Khana wa Botwana.

Wengine ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Yemi Osinbajo, Rais Mohammed Abdullahi Farmajo wa Somalia, Marais wa Gabon, Djibouti, Namibia  na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki. 

Katika hotuba yake baada ya kuaqpishwa na Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, Rais Kenyatta amesema Kenya imedhihirisha kuwa na mfumo unaoheshimu katqiba na utawala wa sheria kwa vile mahakama ilipotengua ushindi wa chama cha Jubilee katika uchaguzi mkuu, serikali iliheshimu uamuzi huo wa mahakama.

Kenyatta amesema serikali yake itaendelea kudumisha msingi huo muhimu wa kuheshimu utawala wa sheria na amewataka wakeya wote kuheshimu sheria hata kama kuna chuki za aina yoyote kati yao.

Maelfu ya watu wamehudhuria sherehe hizo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment