Responsive image
Responsive image
Posted : November 27, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Jeshi la Zimbabwe
Responsive image

Jeshi la Zimbabwe limesema hali ya utulivu imeanza kurejea katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare na katika miji mingine, baada ya siku kadhaa za maandamano ya kumshinikiza rais wa kwanza kwa nchi hiyo Robert Mugabe kuachia madaraka.

Jeshi hilo limesema askari wa Zimbabwe wameondoka katika mitaa ya mji wa Harare na kuanza kurejea kambini kwa ajili ya majukumu mengine.

Hata hivyo jeshi hilo limetahadharisha kuwa wakati wanajeshi wakiondoka mitaani vyombo vingine vya dola vinatakiwa kushika zamu. Jeshi limesema kumekuwa na matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakiendelea kwa mwamvuli wa kushangilia kumuondoa Mugabe madarakani. Baadhi ya watu wameonekana wakipora na kuiba vitu vya watu, huku wengine wakiwavamia watu majumbani na kufanya uhalifu.

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameapishwa kuliongoza taifa hilo na tayari ameanza zoezi la kuchagua baraza lake la mawaziri.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment