Responsive image
Responsive image
Posted : November 26, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Wanajeshi wa Kenya
Responsive image

Jeshi la serikali ya Kenya limesema limefanikiwa kuwafukuza wapiganaji wa kikundi cha Al Shabaab waliokuwa wakijificha katika msitu unaopakana na nchi jirani ya Somalia na kufanya mashambulizi ya kushitukiza.

Wapiganaji hao wamekuwa wakifanya mashambulio dhidi ya wanavijiji wanaoishi karibu na msitu huo na kuwafanya wengi wao kulazimika kuishi katika kambi za wakimbizi.

Hata hivyo licha ya tangazo hilo la jeshi la serikali ya Kenya bado wanavijiji wengi wanaogopa kurejea katika makazi yao jirani na msitu huo.

Watu hao wamesema wana wasi wasi bado usalama wao uko hatarini kwani mara kadhaa wapiganaji wa kikundi cha Al Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulio ya kushitukiza na kusababisha maafa kwa wanavijiji.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment