Responsive image
Responsive image
Posted : November 24, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Dkt. Harrison Mwakyembe
Responsive image

Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye pambano la masumbwi la kuwania ubingwa wa dunia Global Boxing Championship (GBC) katika uzito wa kati ambalo mtanzania Ibrahim Class anamwalika Coos Sibia wa Afrika Kusini katika pambano litakalofanyika kesho Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa kupitia TBC1 ambapo amesema serikali inajivunia kuona vijana wa kitanzania wakifanya vizuri kwenye michezo.

Ili kuhakikisha kizazi kijacho kinaupenda mchezo wa masumbwi, Waziri Mwakyembe ameruhusu wanafunzi wa shule za msingi waingie bure kwenye pambano hilo ambapo wanafunzi hao watatakiwa kuvaa sare za shule ili watambulike wakiambatana na walimu wao.

Kwa upande wake bondia Ibrahim Class amesema amejiandaa vyema kutetea taji hilo alilolitwaa nchini Ujerumani

ENOCK BWIGANE

NOVEMBA 24, 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment