Responsive image
Responsive image
Posted : November 24, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Emmerson Mnangagwa
Responsive image

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo. Maelfu ya watu wamejitokeza katika uwanja wa taifa wa Zimbabwe uliopo mjini Harare kushuhudia kuapishwa kwa kiongozi huyo.

Mnangagwa anakuwa Rais wa pili wa Zimbabwe ambapo rais wa kwanza wa nchi hiyo Robert Mugabe alitangaza kujiuzulu wadhifa wake siku ya jumanne.

Wananchi waliohudhuria kwenye sherehe hizo katika uwanja wa taifa wenye uwezo wa kubeba watu elfu sitini wamesema wana matumaini na rais huyo mpya.

Sherehe hizo zimehuduriwa na viongozi waliopo madarakani na viongozi wastaafu kutoka mataifa mbalimbali barani afrika.

Kiongozi huyo anatarajiwa kuiongoza Zimbabwe wakati taifa hilo likiendelea kujiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani. Jana Mnangagwa aliwasili mjini harare akitokea afrika kusini alikokimbilia baada ya Mugabe kumfukuza kazi.

Jumanne wiki hii mugabe alikabidhi barua ya kujiuzulu wadhifa wake katika bunge la nchi hiyo.

Rais huyo wa kwanza wa Zimbabwe, amepatiwa kinga ya kutoshitakiwa ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa kati yake na uongozi wa serikali ya nchi hiyo ili aweze kuachia madaraka na kupisha uongozi mwingine.

Kutokana na kinga hiyo Mugabe sasa anaweza kuendelea kuishi nchini mwake Zimbabwe na hana ulazima wa kwenda kuishi uhamishoni.

 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment