Responsive image
Responsive image
Posted : November 23, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya wachezaji timu ya taifa ya vijana wenye ulemavu wa macho
Responsive image

Watanzania wameombwa kuichangia  timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa watu wenye ulemavu wa macho na wenye uoni hafifu, ili wapate  vifaa vitakavyotumika katika mchezo wa  goalball.

Akizungumza na TBC baada ya kuwasili kwa wachezaji wa timu hiyo ya Taifa waliokuwa jijini Kampala, Uganda katika mashindano ya Afrika mashariki, kocha wa timu hiyo Mariam Mtweve amesema pamoja na kufanikiwa kuwa washindi wa tatu katika mashindano hayo, changamoto kubwa inayowakabili  ni ukosefu wa vifaa  huku wachezaji wa kikosi hicho wakiongozwa na nahodha wao Msolomi Mwinyi wakitoa Rai kwa Watanzania kuwaunga mkono. Vijana hawa wanajivunia nafasi ya Tatu waliyoipata katika mashindano hayo ya vijana kwa walemavu wa macho na wenye uoni hafifu.

Katika mashindnao hayo, Vijana kutoka Kenya walibuka mabingwa, wakifuatiwa na Uganda katika nafasi ya pili na Tanzania katika nafasi ya tatu ambapo mataifa Sita yameshiriki , wakiwemo wenyeji Uganda, Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini  Mashindano  hayo yaliyofanyika kwa siku tano.

MARIO CHETO

NOVEMBA 23, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment