Responsive image
Responsive image
Posted : November 20, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Wafuasi wa chama cha Jubilee nchini Kenya wakishangilia mtaani kufuatia maamuzi ya mahakama ya juu ya nchi hiyo kutupilia mbali kesi iliyokuwa ikipinga matokeo ya uchaguzi wa marudio uliofanyika oktoba 26 mwaka huu.
Responsive image

Rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo tarehe 28 mwezi huu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kutupilia mbali kesi iliyokuwa ikipinga matokeo ya uchaguzi wa marudio uliofanyika oktoba 26 mwaka huu.

 

Mara baada ya uamuzi huo wafuasi wa Chama cha Jubilee wameonekana katika baadhi ya mitaa wakiandamana kufurahia uamuzi huo, huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika maeneo ya Kisumu na Nairobi.

 

Uamuzi wa mahakama uliotangazwa na Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga umehalalisha ushindi wa Uhuru Kenyatta  ambae tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya (IEBC) ilimtangaza mshindi wa uchaguzi huo wa marudio.

 

Jaji Maraga amesema jopo la majaji limetafakari maombi ya walalamikaji pamoja na aya za katiba katika kufikia uamuzi wake, ambapo wameona kuwa malalamiko hayo hayana msingi.

 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment