Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Viongozi wa CCM mkoa wa Simiyu
Responsive image

Baadhi ya wabunge mkoani Simiyu wameahidi kushirikiana na Rais John Pombe Magufuli katika juhudi za kuwaletea maendeleo wananchi  sambamba na kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano ya viwanda.

 

Wakizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi wa diwani kata ya Nyabubinza wilayani Maswa wakati wakimnadi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Emmanuel Ndalawa wabunge hao wameahidi kumuunga mkono Rais Magufuli katika suala la maendeleo kwa wananchi.

 

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Simiyu Dkt Titus Kamani  amewasisitiza wananchi wa kata ya Nyabubinza  kujitokeza kwa wingi Novemba 26 mwaka huu, kumchagua mgombea wa chama cha mapinduzi ili kutekeleza ilani ya chama hicho kwa vitendo.

 

 

PASCHAL MICHAEL

13 NOVEMBA 2017. 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment