Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Madiwani wa Halmashauri ya Newala
Responsive image

Madiwani halmashauri ya wilaya ya Newala mkoani Mtwara wameelezea masikitiko yao ya kukosekana kwa soko la Mbaazi na kusababisha halmashauri hiyo kukosa mapato.

 

Wakizungumza kwenye kikao cha baraza hilo, wamesema robo ya kwanza ya mwaka 2016 kipindi kama hiki walikusanya ushuru zaidi ya shilingi milioni 100, lakini robo ya mwaka huu wamekusanya shilingi milioni 12.  

 

Diwani wa Kata ya Mtunguru CHITWANGA NDEMBO  amesema miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na kukosekana kwa soko la zao la mbaazi hali iliyosababisha halmashauri hiyo kukosa mapato kama walivyokusudia.

 

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Mussa Chimae amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema itarudisha nyuma umaliziaji wa miradi ya maendeleo.

 

 

MARTINA NGULUMBI

13 NOVEMBA 2017. 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionSalum  |  6 months ago   |   November 20, 2017
"habali zenu"

Leave Your Comment