Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Wananchi wa Kijiji cha Ilembo Kata ya Vwawa Wilaya ya Mbozi
Responsive image

Wananchi wa Kijiji cha Ilembo Kata ya Vwawa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wamelezea kutoridhishwa na matumizi ya zaidi ya Shilingi Milioni Nane zilizotumika kukarabati zahanati ya kijiji chao

 

Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliotishwa na Mwenyekiti wa Halmashauriya Wilaya ya Mbozi, Erick Minga wamesema fedha iliyotumika hailingani na thamani ya ukarabati huo na hivyo amefanyika kufanyika kwa uchunguzi wa tuhuma hizo kauli iliyoungwa mkono na wananchi

 

Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Ilembo, Jackson Mwazembe ametoa malalamiko yake juu ya hofu ya matumizi yasiyo sahihi akisema hailingani na kazi halisi ya ukarabati wa zahanati yao kutokana na wananchi kuchangia nguvu zao.

 

Ukarabati wa zahanati hiyo unafuatia mkakati wa serikali wa kuboresha huduma za afya katika jamii hasa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

 

 

AINESS  THOBIAS

13 NOVEMBA 2017. 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment