Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. GEORGE MKUCHIKA
Responsive image

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, GEORGE MKUCHIKA amesema serikali haijapata madhara yoyote kujitoa katika Mpango wa Kimataifa wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi  -OGP.

 

Akijibu swali bungeni Mjini DODOMA Waziri MKUCHIKA amesema ipo mipango inayotekelezwa ndani ya nchi inayotosheleza kuendeleza kujijegea uwazi na  uwajibikaji katika utendaji wa shughuli za serikali na  mapambano dhidi ya rushwa.

 

Naye Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ABDALLAH ULEGA amesema serikali itaendelea kutoa elimu kwa wavuvi nchini ili kuweza kutumia zana bora za uvuvi ili  kudhibiti uvuvi haramu na kulinda rasilimali za bahari.

 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji JUMAA AWESO amesema katika kukabiliana na wadaiwa sugu wa madeni ya maji, serikali inaanzisha utaratibu wa kulipia huduma ya maji kabla ya matumizi ili kuongeza makusanyo na kuboresha huduma hizo kwa wananchi.

 

 

GHANIYA JUMBE

13 NOVEMBA 2017.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment