Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Kikosi cha Taifa Stars.
Responsive image

Timu ya taifa ya TANZANIA Taifa Stars imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Benin katika mchezo wa kirafiki wakimataifa uliofanyika mjini Cotonou nchini Benin.

 

Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa nchini humo, hadi mapumziko wenyeji Benin, walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa kwa penalti na mkongwe mwenye umri wa miaka 33, Nahodha, Stephane Sessenyoo anayechezea klabu ya Mon’pellier ya Ufaransa.

 

Kipindi cha pili, Tanzania ilianza kwa nguvu na kasi zaidi wakishambulia kutokea pembeni na hatimaye kufanikiwa kupata bao la kusawazisha.

 

Benin imeshindwa kulipa kisasi kwa Tanzania, kwani mara ya mwisho, zilipokutana Oktoba 12, mwaka 2014 Taifa Stars ilishinda 4-1, mabao yakifungwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kiungo Amri Kiemba ,Thomas Ulimwengu na Juma Luizio.

 

 

OSCAR URASSA 

13 NOVEMBA 2017.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionLEONCE V. CHERU  |  5 months ago   |   December 07, 2017
"Sters nawatakia maandalizi mema ya sekafa"

Leave Your Comment