Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Kocha wa timu ya taifa ya Ireland ya Kaskazini, Michael O'neill.
Responsive image

Kocha wa timu ya taifa ya Ireland ya Kaskazini  Michael O'neill anasema kampeni zao za kufuzu kwa fainali za kombe la dunia nchini Rusia mwakani zimemalizika kwa mafanikio makubwa licha ya kuishia kwenye hatua ya mtoano na kushindwa kufuzu.

 

Matokeo ya kutofungana katika mchezo wa marudiano jana usiku mjini Basel mbele ya wenyeji Swizland hayakutosha kuwavusha Ireland Ya Kaskszini kwani katika mchezo wa kwnza walilala bao moja kwa bila nyumbani na O’neill anasema kwa hakika kila mchezaji alipamabana kadiri ya uwezo wake na kila kitu kimefikia mwisho.

 

Swizland wanafuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa ushindi wa jumla wa goli moja kwa bila na kuungana na Croatia ambao nao wamefuzu kwa ushindi wa jumla wa magoli manne kwa Moja dhidi ya Ugiriki ushindi huo waliupata katika mchezo wa kwanza nyumbani mjini Zagreb.

 

Hii leo mabingwa wa mwaka 2006 Italia wanakibarua cha kupindua matokeo mbele ya Sweden katika mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye dimba la San Siro mjini Milan.

 

Katika mchezo wa kwanza Italia wakiwa ugenini mjini Stockholm, Sweden walinyukwa bao moja kwa bila hivyo ili wafanikiwe kufuzu kwa fainali za kombe la dunia ni lazima wawashinde Sweden kwa zaidi ya goli mbili.

 

 

OSCAR URASSA

13 NOVEMBA 2017.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment