Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Toronto Raptors inayoshiriki ligi ya NBA ya nchini Marekani
Responsive image

Katika ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu nchini Marekani ya NBA alfajiri ya leo kumechezwa michezo minne ambapo Toronto Raptors wakiwa ugenini pale TD GARDEN mjini Boston, Miami katika moja ya michezo migumu wamepoteza kwa tabu baada ya kulala kwa alama 95 kwa 94 mbele ya wenyeji Boston Celtics.

 

Licha ya nyota wa Raptors kufunga alama 24 peke yake lakini hazikutosha kuwaokoa na kipigo hicho kilichochagizwa na alama 21 za kwake Al Horford samabamba na Jeylon Brown aliyefunga alama 18 na kuifanya CELTICS kuzima mbwembwe za Raptors toka Canada.

 

Katika matokeo mengine Detroit Pistons wakiwa nyumbani kwenye dimba la Little Caesars mjini Detroit, Miami wametoa dozi baada ya kuwashushia Miami Heat kipigo cha alama 112 kwa 103.

 

 

OSCAR JOSHUA

13 NOVEMBA 2017.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment