Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Dereva mashuhuri wa kampuni ya Ferrari Sebastian Vettel
Responsive image

Dereva mashuhuri wa kampuni ya Ferrari Sebastian Vettel ameshinda shindano lake la kwanza tangu mwezi July baada ya kuibuka kinara katika michuano ya Brazilian Grand Pri, ambayo imeshudia bingwa wa dunia Lewis Hamilton akishindwa kufanya vyema na kumaliza katika nafasi ya nne.

 

Hamilton, ambaye wiki iliyopita alijinyakulia taji lake la nne la dunia kwenye mashindano ya Mexico, aliwashangaza wengi baada ya kuachwa mkiani wakati mbio zikianza lakini baadae alipambana hadi kumaliza katika nafasi ya nne.

 

Mashindano ya jana ya Brazilian Grand Pri yalikuwa ya mwisho kwa dereva wa kampuni ya Williams, Felipe Massa ambaye ametangaza kustaafu rasmi mbio za langalanga na jana amemaliza katika nafasi ya saba huku akishika nafasi ya kumi kwenye msimamo wa mbio za langa langa kwa mwaka huu.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment