Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Elizabeth Michael akiwa mahakamani na mama yake.
Responsive image

Mahakama Kuu Kanda ya DSM imemuhukumu msanii wa filamu nchini, ELIZABETH MICHAEL maarufu LULU kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii STEVEN KANUMBA.

 

Hukumu iliyosomwa na Jaji SAM RUMANYIKA imemtia hatiani LULU kuwa alimuua msanii mwenzake, Marehemu STEVEN KANUMBA bila kukusudia usiku wa Aprili 7, 2012 SINZA Jijini DSM.

 

Wakili wa LULU, PETER KIBATALA anasema wanajipanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

 

 

GHANIYA JUMBE

13 NOVEMBA 2017.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment