Responsive image
Responsive image
Posted : November 09, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Shirika la Utangazaji Tanzania
Responsive image

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linawataarifu wakazi wa Dodoma Mjini kuwa matangazo ya TBC Taifa katika masafa 87.7 na TBC FM katika masafa ya 90.4 yamezimwa.

Hatua hii ni kwa ajili ya kupisha ukarabati mkubwa wa minara unaoendelea. Matangazo yatarejea mara tu baada ya kukamilika kwa matengenezo.

Wakati huo huo katika kuboresha matangazo ya TV na Redio, TBC imefanya maboresho kwenye mtambo wake wa kurushia matangazo.

Hivyo kama hupati matangazo ya TBC kwa wanaopokea matangazo moja kwa moja kutoka mtambo wa TBC Mikocheni, wanatakiwa ku-retune upya visimbuzi vyao.

Tangazo hili haliwahusu wanaopokea matangazo ya TBC kupitia visimbuzi vya Startimes, DSTV, Azam, Digitech, Continental na Agape.

Hakuna badiliko lolote la masafa (frequency)

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment