Responsive image
Responsive image
Posted : November 08, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Wanafunzi sita wa  shule ya msingi Kihinga wilayani Ngara mkoani Kagera  wamekufa na wengine 24 kujeruhiwa baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu kulipuka.

 

Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngara Aidan Bahame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

Akielezea tukio hilo diwani wa kata ya Kibogora wilayani Ngara, Adronis Bulindoli amesema kuwa kitu hicho kimelipuka muda mfupi kabla ya wanafunzi hao kuingia darasani.

 

Kati ya hao  wanafunzi Watatu, wamefariki pale pale na wengine wawili wamekufa wakiwa njiani kupelekwa katika hospitali ya misheni ya Rulenge na mmoja amekufa wakati akipatiwa matibabu.

 

Kwa upande wake  mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Ngara Erick Nkilamachumu amesema wauguzi wa hospitali ya Rulenge wanaendelea na jitihada za kuokoa maisha ya wanafunzi waliojeruhiwa.

 

Shule ya msingi Kihinga iko mpakani na Burundi ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanadai huenda bomu hilo lililetwa na wanafunzi wanaokuja shuleni kuuza vyuma chakavu.

 

 

CHARLES MWEBEYA

NOVEMBA 08, 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment