Responsive image
Responsive image
Posted : November 08, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila MkumboKatibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo.
Responsive image

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amewataka Wadau wa Maji kushirikiana na Serikali kuhakikisha wananchi wanafikiwa na miradi ili kupata maji ya uhakika hususani maeneo ya vijijini.

 

Prof Kitila ameyasema hayo Mkoani Arusha wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa watalamu wa Maji wa Shirika lisilola Kiserikali la World Vision.

 

Pia amewaomba wadau hao kutoa elimu kwa wananchi juu ya ulinzi wa vyanzo vya maji.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la World Vision Devocatus Kamara amesema miradi ya maji inagharama kubwa hivyo ni vyema kutoa elimu kwa Vikundi vya watumiaji maji na Wananchi ili kufikia lengo tarajiwa.

Shirika la World Vision ni Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na miradi ya maji vijijini pamoja na elimu kwa  watoto wa kike katika mikoa mbalimbali nchini.

 

 

SECHELELA KONGOLA

NOVEMBA 08, 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment