Responsive image
Responsive image
Posted : November 08, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Responsive image

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko serikalini.

 

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo mjini Dodoma wakati akifungua Kikao Kazi cha Baraza la Mawaziri na kubainisha kuwa ni vema  viongozi hao kabla ya kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo halitaleta athari za kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za wizara zao.

 

Pia amewataka wafanye ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

 

Waziri Mkuu amesema Mawaziri na Naibu Mawaziri wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021. 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment