Responsive image
Responsive image
Posted : November 08, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo
Responsive image

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jafo, amesema ofisi yake itahakikisha ahadi zilizotolewa na Rais Joh Magufuli za ujenzi wa barabara za lami katika maeneo mbalimbali nchini zinatekelezwa.

 

Akizungumza bungeni Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu, Waziri Jafo amesema wizara yake ina takwimu zote zilizotolewa na Rais Magufuli wakati wa kampeni ya urais na hivyo wana jukumu la kusimamia utekelezwaji wake.

  

Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema Rais Magufuli hafanyi kazi kwa upendeleo wowote wa kikanda kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya watu, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akifafanua kuwa sheria za nchini zinaruhusu kufanyika kwa shughuli karibu na vyanzo vya maji baada ya kupata kibali maalumu.

 

Waziri Makamba ametoa ufafanuzi huo kufuatia baadhi ya wananchi kukariri vibaya kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa Wilayani Karagwe Mkoani Kagera kuhusu kuruhusu watu kufanya shughuli zao karibu na vyanzo vya maji.

 

 

EDWARD KONDELA

NOVEMBA 08, 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment