Responsive image
Responsive image
Posted : November 01, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli ziarani mkoani Mwanza
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli ametoa wiki mbili kwa wawekezaji wa kiwanda cha Keko na Tanzania Pharmaceutical – TPI vya jijini Dar Es Salaam kuanza uzalishaji mara moja vinginevyo serikali itawanyang’anya viwanda hivyo na kuwapa wawekezaji wengine.

 

Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati akifungua kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical kilichoko Buhongwa jijini Mwanza na kusema uamuzi huo umelenga kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini.

 

Rais Magufuli ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuzalisha dawa zenye ubora ili kukidhi mahitaji ya soko.

 

Kiwanda hicho cha dawa ambacho ni cha kwanza katika mikoa ya kanda ya ziwa kimegharimu shilingi bilioni mbili na tayari kimeajiri wafanyakazi 126.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kiwanda hicho Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kumepunguza adha ya kuagiza dawa kutoka nje ya nchi.

 

Akiwa ziarani mkoani Mwanza Rais Magufuli amepata fursa ya kuzindua kiwanda cha kutengeneza bidhaa za plastiki na vifungashio cha Victoria Moulders na kuwahakikishia wawekezaji kuhusu upatikanaji wa nishati ya uhakika ya umeme.

 

Kiwanda hicho ambacho bidhaa zake zinauzwa ndani na nje ya nchi kimeajiri watanzania mia tano.

 

 

REGINALD NDESIKA

NOVEMBA 01, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment