Responsive image
Responsive image
Posted : October 23, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Prof. Florens Luoga Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania
Responsive image

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Prof. Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ambapo ataanza kazi rasmi baada ya kustaafu kwa Gavana wa sasa Prof. Benno Ndulu.

Rais Mafufuli amefanya uteuzi huo alipokuwa akiwatunuku vyeti watanzania wajumbe walioshiriki kufanya tathmini ya makinikia yaliyokuwa kwenye mchanga wa madini. 

Miongoni mwa waliotunukiwa vyeti ni Spika wa Bunge Job Ndugai ambaye cheti chake kimepokelewa kwa niaba yake na Mke wake Fatma Ndugai.

Sambamba na hayo Rais Dkt. Magufuli amewataka waandishi wa habari kuwa wazalendo ili kuhakikisha ujumbe wanaoutoa unakuwa na manufaa kwa wananchi.

 

GODFRIEND MBUYA

0CTOBA 23, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment