Responsive image
Responsive image
Posted : October 23, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli asubuhi atawatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold.

 

Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini.

 

Kampuni hiyo pia inalipa takribani Shilingi Bilioni 700 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.

 

Tukio hilo litafanyika Ikulu Jijini Dar es salaam  kuanzia saa tano asubuhi ambapo Shirika la Utangazaji Tanzania – TBC kupitia vyombo vyake vya Televisheni na Radio na mtandao wqa  kijamii wa facebook tbc habari itakuletea matangazo hayo moja kwa moja.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment