Responsive image
Responsive image
Posted : October 22, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa Mkoa wa DSM PAUL MAKONDA akiwa kwenye moja ya magari yaliyotengenezwa
Responsive image

Mkuu wa Mkoa wa DSM PAUL MAKONDA amekabidhiwa magari 15 ya polisi yaliyokuwa yakitengenezwa Mkoani Kilimanjaro.

MAKONDA amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuona changamoto zilizokuwa zikiwakabili polisi katika mkoa wake kutokana na aina ya magari waliyokuwa wanatumia.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya DSM, LAZARO MAMBO SASA amesema kuwa uvumbuzi wa tatizo hilo la magari utasaidia katika doria na ukaguzi wa polisi kwani yametengenezwa maalumu kwa kazi hiyo.

Naye Mkurugenzi wa RSA, MANMOHAM BHAMRAH amesema anamshukuru Mkuu wa Mkoa wa DSM PAUL MAKONDA kwa kumpa nafasi hiyo ya kutengeneza magari kupitia kampuni yake.

 Magari ishirini na sita yalipelekwa mkoani Kilimanjaoro kwa jaili ya matengenezo ambapo magari 15 yamepona kabisa na tayari yamekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa huku magari 11 yakishindikana.

Doreen Mlay,

22 Oktoba 2017.

===========

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment