Responsive image
Responsive image
Posted : October 13, 2017 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Selemani Jafo
Responsive image

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Selemani Jafo amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha halmashauri zinazodaiwa na bodi hiyo kwa muda mrefu kuhakikisha zimerejesha fedha hizo ifikapo Desemba 30 mwaka huu.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa Halmashauri 12 nchini hazijarejesha mikopo ya zaidi ya Shilingi Bilioni mbili jambo ambalo limesababisha halmasahauri nyingine kushindwa kukopeshwa.

Waziri Jafo amesema halmashauri hizo zinadaiwa zinadaiwa na bodi hiyo zaidi ya Shilingi Bilioni mbili.

Richard Mfugale ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa nchini anatoa wito kwa halmashauri hizo kurejesha mikopo hiyo.

Hadi septemba 30, mwaka huu Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa nchini imekwisha toa mikopo yenye thamani ya zaidi Shilingi Bilioni tisa nukta saba kwa halmashauri 54 nchini.

 

ANETH ANDREW

OCTOBA 13, 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment