Responsive image
Responsive image
Posted : October 12, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli alipokuwa akimkaribisha Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan Ikulu Jijini Dar es salaam
Responsive image

Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan amesema Jumuiya hiyo itapanua hospitali ya Aga Khan iliyopo Jijini DSM na kujenga chuo kikuu kikubwa Afrika Mashariki, Mkoani Arusha.

 

Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan amesema hayo Ikulu Jijini Dar es salaam  alipofanya mazungumzo na Rais wa Dkt. John Magufuli.

 

Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan amesema Upanuzi wa hospitali ya Aga Khan utahusisha kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa kutoka 72 vya sasa hadi kufikia vitanda 172, utaimarisha matibabu ya moyo na kansa na utaongeza ufundishaji wa madaktari na wataalamu wengine wa afya.

 

Pia Mtukufu Karim Al-Hussaini amesema yeye haamini kuwa ni kipaumbele kwa vyombo vya habari kujikita katika masuala ya siasa na badala yake anaamini kuwa vyombo vya habari vina wajibu mpana zaidi wa kujikita katika masuala ya maendeleo.

 

Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan kwa taasisi zake kutoa huduma za kijamii ikiwemo tiba na elimu.

 

Aidha Rais Magufuli ametoa wito kwa taasisi hizo kupunguza gharama za huduma zake kwa wananchi ili waweze kumudu hasa ikizingatiwa kuwa zimekuwa zikipata msamaha wa kodi kutoka Serikalini.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment