Responsive image
Responsive image
Posted : October 10, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Kiongozi mkuu wa upinzani wa muungano wa NASA nchini Kenya Raila Odinga
Responsive image

Kiongozi mkuu wa upinzani  wa muungano wa NASA nchini Kenya Raila Odinga, ametangaza kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao unapangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

Bwana Odinga amesema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu

Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Aidha Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC, muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia iliyo nzuri.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment