Responsive image
Responsive image
Posted : October 10, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifanya mazungumzo na balozi mpya wa Uganda hapa nchini Richard Kabonero
Responsive image

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Uganda kwa kutafiti na kugundua mafuta kwa kutumia wataalamu wazawa.

Makamu wa rais amesema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na balozi mpya wa Uganda hapa nchini Richard Kabonero aliyefika kujitambulisha.

Naye Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Kabonero amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania ikiwemo masuala ya  tafiti za mafuta zinazoendelea katika ziwa Eyasi, mashirikiano ya sekta ya anga ili kusaidia kukuza utalii, mradi wa ujenzi ya reli ya kati na mradi wa umeme vijijini pamoja na kuanzishwa kwa jukwaa la biashara la sekta binafsi.

Makamu wa Rais alimalizia mazungumzo yake na Balozi huyo wa Uganda hapa nchini kwa kutoa shukrani zake za dhati kwa Rais Yoweri Museveni kwa ushirikiano wake walioutoa wakati wa ajali mbaya ya gari iliyowakuta Watanzania waliokuwa wanatoka Harusini ambapo watanzania 13 walifariki.

Wakati huohuo Makamu wa Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba hapa Lucas Hernandez.

Balozi huyo amesema kuna zaidi ya wataalamu 50 kutoka Cuba wapo nchini katika kusaidia katika Nyanja mbalimbali ikiwemo afya na elimu.

Makamu wa Rais amemaliza mazungumzo yake na Balozi wa Iran nchini Moussa Farhang ambaye ameshukuru mahusiano yaliodumu kwa miaka 40 katika masuala ya tamaduni na  uchumi ikiwemo kilimo, afya, viwanda, gesi na biashara.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment