Responsive image
Responsive image
Posted : October 10, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya siku ya chakula duniani
Responsive image

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeboresha sekta ya kilimo na kuifanya Zanzibar kuwa na chakula kinachojitosheleza.

Rais Dkt. Shein ameyasema hayo mjini Unguja wakati wa uzinduzi wa maonesho ya siku ya chakula duniani ambapo amesema maboresho hayo yameongeza kasi ya uzalishaji katika zao la mpunga baada ya kuvuna tani elfu thelathini na tisa mwaka 2017 kutoka tani elfu thelathini na tatu mwaka 2013.

Amesema lengo la serikali ni kuongeza mavuno na kuondokana na utegemezi wa mchele kutoka nje ya nchi ambapo hivi sasa wastani wa tani za mchele zaidi ya elfu saba zinatoka nje ya nchi.

Rais Dkt Shein ametoa wito kwa wakulima kutumia teknolojia ya kilimo shadidi ili  kuongeza uzalishaji.

Uzinduzi wa maonesho hayo umefanyika ikiwa  ni kuelekea siku ya chakula duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Octoba 16.

 

SWAUMU MAVURA

OCTOBA 10, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment