Responsive image
Responsive image
Posted : October 09, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Rais John Magufuli
Responsive image

Rais John Magufuli  amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na kusema kuwa amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 12 waliopoteza maisha  baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika Ziwa Victoria

Rais Magufuli amemuomba Mongella kumfikisha salamu zake za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliopatwa na msiba huo na anaungana nao katika kuomboleza msiba huo.

Amewaomba kuwa na moyo wa uvumilivu, ustahimilivu na subira katika kipindi hiki cha majonzi.

Rais Magufuli pia amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi na majeruhi walionusurika katika ajali hiyo wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment