Responsive image
Responsive image
Posted : October 09, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Wananchi wakiwa wanashuhudia gari aina ya Hiace ambalo limetolewa katika ziwa Victoria baada ya kutumbukia humo na kusababisha vifo vya watu 12
Responsive image

Watu kumi na wawili wamekufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika Ziwa Victoria kufuatia dereva wa gari hilo lililokuwa katika mwendo mkali kushindwa kulidhibiti katika Kivuko cha Kigong’o Busisi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.

Gari hilo lililokuwa likitokea Buhongwa kwenda Kivukoni Kingon’go Busisi linadaiwa breki zake kushindwa kufanya kazi na hivyo kutumbukia kwenye maji likiwa na idadi ya abiria wanaokisiwa kuwa 17.

Akielezea chanzo cha ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema gari hilo lilikuwa katika mwendo kasi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amesema ajali hiyo ni kubwa na amewataka wananchi kuwa watulivu wakisubiri uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo.

Kwa mujibu wa Meneja wa wakala wa ufundi na Umeme -TEMESA Mkoa wa Mwanza Ferdinand Mshana, hii ni ajali ya sita kutokea katika Kivuko cha Kingon’go Busisi Mkoani Mwanza.

 

REGINALD NDESIKA

OCTOBA 09, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment