Responsive image
Responsive image
Posted : October 09, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli hii leo Octoba 09, 2017 amewaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es saam.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Dkt. Magufuli kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri,kwa kuongeza idadi ya wizara, kuteua Mawaziri na manaibu waziri wapya na kuwahamisha wizara baadhi ya mawaziri na manaibu waziri.

Aidha Rais Magufuli amemuapisha Steven Kagaigai  kuwa Katibu wa Bunge baada ya kuchukua nafasi ya Dkt. Thomas Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Octoba 7 mwaka huu Rais Dkt. Magufuli ametangaza kuongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21, na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21.

Baada ya wateule hao kula kiapo Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka kufanya kazi kwa bidiii katika kuwatumikia wananchi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment